TAARIFA KWA UMMA WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021

           


            TAARIFA KWA UMMA

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2021

 

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

 

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 10 June 2021.

 

Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa, na Makutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

 

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.


Bonyeza hapa I'll kufungua majina katika vituo mbalimbali ndani ya Tz

Comments

Popular posts from this blog

Thing to NOTE;Never Say These 5 Phrases to Your Children,Psychologist warn it.

HESLB Orodha ya waombaji mikopo wanaotakiwa kufanya marekebisho-Postgraduate Loan applicants 2019/2020