MOTIVATION PAGE..... UNLOCK AND LIVE YOUR DREAMS.
UNLOCK AND LIVE YOUR DREAMS
Success 🔑 #03: Kata mnyororo na watu wenye kutafuta makosa katika kila jambo unalolifanya (Cut the chain of faults finders).
Watafuta makosa/wakosoaji (faults finders) ni watu ambao kazi yao wakati wote ni kumkatisha mtu tamaa katika jambo lolote analolifanya. Hata kama mtu akijitahidi namna gani, wao watatafuta kasoro fulani tu ili kumkosoa (critism reason). Mara utasikia wakisema, yule hawezi kitu, pale ameanza tu, lakini hafiki mbali, zile ni nguvu za soda au kawaida yake ni kushindwa. Midomo yao imejaa maneno hasi yenye kukatisha taama na kuvunja moyo.
Kuna msemo usemao, "Faults finders, will even find faults in paradise", yaani hata paradiso watu wakosoaji hutafuta makosa ili wakosoe tu.
Kwanini ukate mnyororo nao?
1. Hujifanya wao ni watabiri wa mafanikio ya wengine (success predictors), hivyo kutokana na kauli zao za kukatisha tamaa, humfanya mtu ajijengee mtazamo duni juu ya uwezo wake.
2. Wao ni watu wa kulaumu, kukosoa na kusengenya tu.Neno hongera haliwezi katu kutoka vinywani mwao.
3. Hujifanya wao ndio wajanja, wajuaji juu ya kila kitu, hivyo hawawezi kukubali mtu mwingine kuwa anaweza.
4. Huwezi katu kujifunza vitu chanya kutoka kwao.
5. Furaha yao ni kukuona wewe ukefeli au ukishimdwa kila mara, ndio mara watakukatisha tamaa ili uendelee kubaki katika hiyo hali.
#Dawa, yao ni kukata mnyororo nao, kujenga uhusiano na watu wenye kuona mambo mazuri juu yako, na kukushauri urekebishe makosa yako ili uweze kusonga mbele zaidi.
Je, wewe ni faults finder kwa wengine, au umezungukwa na faults finders katika maisha yako yako ya kila siku? Uamuzi wako ni upi?
By Emma kehogo
0768782509📞
#Ijue na kuishi Ndoto yako.

Comments
Post a Comment